Masharti na Vigezo vya Matumizi (KKKT DMP)

Imesasishwa mara ya mwisho: April 2026

Kwa kufungua akaunti, kujisajili, au kushiriki katika mfumo wa kidijitali wa mkutano, unakubali kufuata na kuheshimu Masharti na Vigezo hivi pamoja na sera zote zinazohusiana na matumizi ya mfumo huu.

1. Matumizi ya Mfumo

Mfumo huu umetengenezwa mahsusi kwa ajili ya kurahisisha usajili wa washiriki, uthibitishaji wa mahudhurio, mawasiliano kati ya washiriki na waandaaji, pamoja na upatikanaji wa nyaraka na taarifa za mkutano. Matumizi ya mfumo huu nje ya madhumuni yaliyokusudiwa hayaruhusiwi.

2. Usahihi wa Taarifa

Mtumiaji anatakiwa kutoa taarifa sahihi, kamili na za kisasa wakati wa usajili na matumizi ya mfumo. Kutoa taarifa za uongo, zisizo sahihi au zinazopotosha kunaweza kusababisha kusimamishwa au kufutwa kwa akaunti bila taarifa ya awali.

3. Usalama wa Akaunti

Mtumiaji anawajibika kulinda taarifa zake za kuingia (jina la mtumiaji na nenosiri). Hairuhusiwi kushiriki taarifa hizi na mtu mwingine yeyote. Waandaaji wa mfumo hawatawajibika kwa madhara yatokanayo na matumizi mabaya ya akaunti yaliyosababishwa na uzembe wa mtumiaji.

4. Ufuatiliaji wa Mahudhurio

Mahudhurio ya mkutano yatathibitishwa kupitia skanning ya QR Code au njia nyingine za kidijitali zilizoidhinishwa. Taarifa za mahudhurio zitatumika kuthibitisha ushiriki wa mkutano na ustahiki wa kupata vyeti (iwapo vitatolewa).

5. Maudhui ya Mtumiaji

Mtumiaji anawajibika kwa maudhui yote anayowasilisha kwenye mfumo huu, ikiwemo nyaraka, ujumbe wa mazungumzo (chat), picha za wasifu na taarifa nyingine. Hairuhusiwi kupakia au kusambaza maudhui yenye:

Waandaaji wana haki ya kuondoa au kufuta maudhui yoyote yasiyofaa bila taarifa ya awali.

6. Faragha na Matumizi ya Taarifa

Kwa kutumia mfumo huu, unakubali kuwa taarifa zako binafsi zitakusanywa, kuhifadhiwa na kutumika kwa madhumuni ya kuendesha mkutano, ikiwa ni pamoja na usajili, mawasiliano, uthibitishaji wa malipo na utoaji wa huduma zinazohusiana. Taarifa zako hazitashirikishwa na wahusika wa nje bila idhini yako isipokuwa pale inapohitajika kisheria.

7. Usalama wa Mfumo

Ni marufuku kujaribu kuvuruga, kudukua (hack), au kuathiri utendaji wa mfumo kwa namna yoyote. Hatua kali za kinidhamu na kisheria zinaweza kuchukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayehusika na vitendo hivyo.

8. Kanusho (Disclaimer)

Ingawa tunajitahidi kuhakikisha mfumo unafanya kazi kwa ufanisi na bila hitilafu, hatuwezi kutoa dhamana ya upatikanaji wa huduma bila kukatika au makosa ya kiufundi. Hatutawajibika kwa hasara yoyote itakayotokana na:

9. Kusimamishwa au Kufutwa kwa Akaunti

Waandaaji wana haki ya kusimamisha au kufuta akaunti ya mtumiaji yeyote atakayekiuka masharti haya, au atakayejihusisha na matumizi mabaya ya mfumo bila kutoa taarifa ya awali.

10. Mabadiliko ya Masharti

Masharti haya yanaweza kubadilishwa au kusasishwa wakati wowote kulingana na mahitaji ya mfumo au mkutano. Mtumiaji anawajibika kupitia masharti haya mara kwa mara ili kujua mabadiliko yoyote yaliyofanyika.

11. Mawasiliano

Kwa maswali, maoni au msaada, tafadhali wasiliana na waandaaji wa mkutano kupitia njia rasmi za mawasiliano zilizotolewa.